Freelancers & Watoa Huduma

Umechoka kulipa kabla ya kupata huduma?
Au kufanya kazi bila malipo?

Enpay.app ni suluhisho la malipo salama (escrow) kwa matumizi tofauti ya kila siku. Hakuna kubahatisha. Hakuna kuamini kwa maneno. Linda pesa yako leo.

Jinsi Inavyofanya Kazi kwa Freelancers

1

Mteja anaweka pesa

Mteja anakuundia escrow na kuweka pesa ndani. Wewe unaona kuwa pesa ipo kabla hujaanza.

2

Unafanya kazi

Unafanya kazi kwa uhakika kuwa malipo yako yamesubiri. Kama ni mradi mkubwa, unalipwa kwa hatua (milestones).

3

Unapokea malipo yako

Baada ya mteja kukubali kazi imekamilika, pesa inatolewa moja kwa moja kwenye wallet yako.

Kwa nini Enpay ni bora kwa freelancers?

Mteja anaweka pesa kwanza

Hakuna kazi bila malipo. Pesa inawekwa kwenye escrow kabla hujaanza.

Unafanya kazi kwa uhakika

Una uhakika kuwa malipo yako yamesubiri. Fanya kazi bila wasiwasi.

Malipo baada ya kukamilisha

Baada ya kukubaliana na mteja kuwa kazi imekamilika, pesa inatolewa kwako.

Milestone payments

Gawa kazi yako katika hatua. Kila hatua ikikamilika, unalipwa sehemu ya pesa.

Muda wa dispute ni masaa 48

Kama kuna hitilafu, timu yetu inasuluhisha ndani ya masaa 48.

Reputation system

Kila mteja anakupa rating. Reputation yako inakuwa sifa ya kazi zako zijazo.

Maswali Yanayoulizwa Sana

Je, ni aina gani za kazi zinaweza kutumia escrow?

Aina zote za kazi za freelancing — uandishi, kubuni (design), programu (coding), tafsiri, masomo, ushauri, na nyinginezo. Kwa kuwa escrow ina support milestones, unaweza kugawa mradi wako katika hatua ndogo.

Je, mteja anaweza kurudisha pesa baada ya kazi kuanza?

Hapana. Pesa inakuwa imefungwa kwenye escrow. Inaweza kutolewa tu baada ya kazi kukamilika au kwa makubaliano ya pande zote mbili. Kama kuna mgogoro, timu yetu inasuluhisha.

Je, kuna ada kwa freelancers?

Hakuna ada za kutumia Enpay kwa freelancers. Wateja wanalipa ada ndogo ya mfumo (1-2%) wanapoweka pesa. Wewe unapokea kiasi kamili cha malipo yako.

Je, ninahitaji KYC kuwa freelancer?

Ndiyo, kwa kufikia kiwango fulani cha mauzo au ukubwa wa mradi, utahitaji kukamilisha KYC. Hii inasaidia kujenga uaminifu kati yako na wateja wako.

Je, ninaweza kuomba malipo kwa TZS?

Ndiyo. Enpay inasaidia TZS (Shilingi za Tanzania) kwa malipo yote. Unaweza kuweka na kutoa pesa kwa njia za M-Pesa, Airtel Money, Tigo Pesa, na Halotel.

Anza sasa kutumia Enpay.app

Fanya biashara, malipo, na mipango yako kwa uhakika. Hakuna kubahatisha.