Kulipa Rent ya Nyumba

Linda pesa yako wakati wa kupanga nyumba

Lipa kodi ya nyumba kupitia Enpay. Pesa inashikiliwa kwenye escrow na kutolewa tu baada ya makubaliano kutimia. Hakuna tena wasiwasi wa “nililipa lakini…”

  • Mpangaji analinda kodi yake
  • Mwenye nyumba anauhakika wa malipo
  • Dispute window ya siku 5 kwa mikataba mikubwa

Jinsi Inavyofanya Kazi kwa Kupanga Nyumba

1

Panga makubaliano

Mpangaji na mwenye nyumba wanakubaliana masharti ya kukodisha. Unda escrow kwa kiasi cha kodi.

2

Lipa kodi escrow

Mpangaji analipa kodi kwenye escrow ya Enpay. Mwenye nyumba anaona pesa ipo kabla hajatoa nyumba.

3

Pesa inatolewa kwa mpangilio

Baada ya muda wa kukodisha kumalizika au makubaliano kutimia, pesa inatolewa kwa mwenye nyumba.

Faida kwa Mpangaji na Mwenye Nyumba

Kwa Mpangaji

  • Pesa yako inalindwa hadi nyumba ipatikane kama ilivyoahidiwa
  • Hakuna hatari ya kupoteza kodi kwa mwenye nyumba ambaye hajamudu
  • Unaweza kufungua dispute kama nyumba haipo kama ilivyoelezwa
  • Muda wa dispute ni hadi siku 5 — wa kutosha kwa mikataba ya nyumba

Kwa Mwenye Nyumba

  • Una uhakika mpangaji ana pesa kabla hajapata nyumba
  • Hakuna wateja wa kutisha — wanaokuja bila uwezo wa kulipa
  • Pesa inatolewa moja kwa moja kwenye wallet yako baada ya mpangilio
  • Reputation system inasaidia kujenga sifa ya mwenye nyumba anayeaminika

Maswali Yanayoulizwa Sana

Je, ninaweza kutumia escrow kulipa kodi ya mwaka mzima?

Ndiyo. Enpay escrow inaweza kushikilia kiasi chochote hadi TZS milioni 100. Unaweza kulipa kodi ya mwaka mzima kwa usalama.

Je, mwenye nyumba anaweza kukataa escrow?

Mwenye nyumba anafaidi pia — anaona kuwa pesa ipo kabla hajatoa nyumba. Escrow inawalinda wote wawili.

Je, kuna ada kwa kulipa kodi kupitia Enpay?

Mpangaji analipa ada ndogo ya mfumo (1-2%) anapoweka pesa. Hakuna ada za ziada.

Je, ninaweza kufanya nini kama nyumba haipo kama ilivyoelezwa?

Fungua dispute kupitia Enpay. Timu yetu inakagua ushahidi na kutoa uamuzi ndani ya siku 5.

Linda kodi yako ya nyumba leo

Enpay.app inahakikisha kila upande uko salama wakati wa kupanga na kukodi nyumba.